Rais Macky Sally wa Senegal amesema kuwa hatafanya mazungumzo ya
aina yoyote na waasi wa eneo la Casamance yenye lengo la kujitenga na
serikali kuu ya nchi hiyo. Akizungumza kwenye kongamano la wakurugenzi
wa vyombo vya habari vya Afrika mjini Dakkar, Rais Sally ameongeza kuwa,
kujitenga eneo la Casamance kamwe jambo halikubaliki na kusisitiza
kwamba Casamance ni sehemu ya ardhi ya Senegal. Ameongeza kuwa, njia
pekee ya kuutatua mgogoro wa eneo hilo lililopo kusini mwa nchi hiyo ni
kuendelezwa mazungumzo kati ya serikali na waasi wa The Movement of
Democratic Forces of Casamance MFDC. Rais wa Senegal amebainisha kuwa,
kufanyika mazungumzo ya wazi kwa shabaha ya kupatikana amani na
uthabiti, kutapelekea kupatikana ustawi na maendeleo ya kiuchumi nchini
humo. Waasi wa Casamance walianza uasi tokea miaka ya 1980 kwa lengo
la kujitenga eneo la kusini mwa nchi hiyo. Inafaa kukumbusha kuwa,
Abdullaye Wade Rais wa zamani wa Senegal alifikia kwenye makubaliano ya
amani na waasi hao wa MFDC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment