skip to main |
skip to sidebar
Wanafunzi USA wapinga ushindi wa Obama
Duru za habari kutoka Marekani zimearifu kuwa, mamia ya wanafunzi
wa chuo kikuu cha Mississippi katika jimbo la Mississipi, wamefanya
maandamano makubwa kupinga ushindi wa Rais Barack Obama. Wanafunzi hao
wanaokadiriwa kufikia 400 walimiminika mabarabarani kupinga hatua ya
kuchaguliwa mara ya pili rais Obama. Chuo kikuu hicho kimetoa ripoti
kuwa, mikusanyiko ya wanafunzi ilianza tangu siku ya Jumanne usiku na
kuongezeka zaidi jana na leo. Wanafunzi hao waliokuwa wamejawa na hasira
walibeba mabango mbalimbali huku wengine wakitoa nara za kulaani
ushindi huo wa Obama. Kufuatia purukushani hizo, polisi walilazimika
kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment