skip to main |
skip to sidebar
UNICEF yalaani utekaji nyara nchini Kongo
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umelaani vikali hatua
ya kukamatwa mateka wafanyakazi wawili wa sekta ya afya katika eneo
linalokumbwa na machafuko la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa ya UNICEF imeeleza kuwa, mhandisi mmoja
anayeshughulikia na masuala ya ustawi wa ujenzi na mwengine mtoa misaada
ya kibinadamu katika jimbo hilo, wamekamatwa mateka na watu wanaobeba
silaha karibu wa mpaka wa nchi hiyo na Uganda. Taarifa hiyo imeongeza
kuwa, wafanyakazi hao wamekamatwa mateka wakati wakitoa chanjo za polio
kwa watoto katika eneo hilo. UNICEF imeeleza kuwa, kutolewa huduma
likiwemo suala la kupatiwa chanjo watoto wadogo, ni miongoni mwa haki za
watoto wote ulimwenguni. Jumla ya watu milioni mbili na nusu
wanakabiliwa na hali mbaya ya kiafya kwenye kambi za wakimbizi zilizopo
kwenye eneo la mashariki mwa Kongo
No comments:
Post a Comment