Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 13, 2012

Marekani yazuia kuchunguzwa haki za binadamu



Marekani yazuia kuchunguzwa haki za binadamu
Serikali ya Marekani inalizuia Baraza la Haki la Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na nchi hiyo sehemu mbalimbali za dunia.
Taarifa zinasema kuwa, kutiwa mbaroni,
kuteswa washikiliwa kwenye jela za kuogofya za Marekani duniani kote na hasa kwenye jela ya Guantanamo na hali kadhalika mauaji dhidi ya wafungwa hao, ni miongoni mwa mambo yaliyolifanya faili la haki za binadamu la Marekani kuwa chafu mno.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Rais Barack Obama wa nchi hiyo mwenyewe hutoa amri ya kuuawa watu katika nchi nyingine na hali kadhalika hutoa amri ya kufanyika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye nchi za Kiislamu. Taarifa zinasema kuwa, Marekani pia inafanya juhudi za kulizuia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lisichunguje jinai na ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

No comments:

Post a Comment