Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa ameonya kuwa iwapo
wapiganaji wa Kisalafi wanaopigana vita dhidi ya serikali ya Rais Bashar
al Assad wataidhibiti Syria, basi nchi hiyo ya Kiarabu itageuka na
kitovu cha mazalio ya magaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. Dakta
Ismail Salami msomi wa Kiirani na mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika
eneo hili amesema ni wazi kuwa wanamgambo wa Kisalafi tayari wapo huko
Syria na wanaendesha mapigano dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad
wa nchi hiyo. Akiashiria wito uliotolewa mwezi Februari mwaka jana na
Ayman al Zawahiri kiongozi wa mtandao wa al Qaida kwa wafuasi wake
akiwataka waendeshe vita dhidi ya Rais wa Syria, Dakta Ismail Salami
amesema kuwa lengo kuu la njama hizo ni kuigeuza Syria kuwa maficho
salama kwa Masalafi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment