Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 27, 2012

Jenerali Nyakairima: Waasi wa M23 kuondoka Goma


Jenerali Nyakairima: Waasi wa M23  kuondoka GomaMkuu wa Majeshi ya Uganda Jenerali  Aronda Nyakairima amesema kuwa, Kanali Sultani Makenga msemaji wa kundi la waasi wa M23 amemthibitishia kwamba, wamekubaliana na mpango wa kuondoka kwenye mji wa Goma wanaoudhibiti kwa muda wa wiki moja, ili kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo na serikali ya Kinshasa.
Jenerali Nyakairima ameongeza kuwa,  Rais Joseph Kabila wa Kongo siku ya Jumamosi tarehe 24 Novemba alikutana na kufanya mazungumzo na mwakilishi wa waasi wa M23 mjini Kampala, Uganda na kuwapa sharti la kuondoka kwanza na kurejea nyuma hadi kwenye mji wa Sake ulioko umbali wa kilomita 20 kutoka Goma kabla ya kufanyika mazungumzo ya amani.
Hivi karibuni, Wakuu wa nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika ICGLR walikutana mjini Kampala, na kuchukua uamuzi wa kuwapa muda wa masaa 48 waasi hao  kuondoka mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini.

No comments:

Post a Comment