
Mripuko wa homa ya manjano huko
katika jimbo la Darfur nchini Sudan umeua watu 107 katika kipindi cha
wiki sita zilizopita. Hayo yameripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
na kutahadharisha kwamba ugonjwa huo huenda ukaenea kote nchini Sudan.
WHO imesema kuwa homa hiyo ya manjano inazidi kuua watu wengi na kwamba
Sudan hivi sasa inafanya juhudi za kupata chanjo ya dharura ya maradhi
hayo. Maafisa wa WHO waliripoti kuwa jumla ya watu 67 wamefariki dunia
kwa maradhi hayo ya homa ya manjano. Hakuna dawa maalumu kwa ugonjwa wa
homa ya manjano inayoenezwa na mbu, bali daktari humhudumia mgonjwa
kulingana na dalili kuu anazokuwa nazo kama vile kuwa na upungufu wa
maji mwilini, homa, kuvuja damu na kutapika. Dakta Ansu Banerjee wa
Ofisi ya WHO huko Sudan amesema kuwa jumla ya dozi milioni 2.4 za chanjo
ya homa ya manjano zinatazamiwa kuwasili Khartoum mji mkuu wa Sudan
wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment