Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amelaani hatua ya
Israel ya kukiuka haki za binadamu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu
za Palestina. Nabil al Arabi amesema hayo leo alipokutana na Richard A.
Falk Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu katika ardhi
zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo
mjini Cairo. Al Arabi amelaani hatua za askari wa Israel za kukiuka
haki za binadamu katika ardhi za Palestina ukiwemo Ukanda wa Gaza na
Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za
Kiarabu pia ameunga mkono aumuzi wa Wapalestina wa kutaka kuwa na
uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa, pendekezo ambalo linatarajiwa
kupigiwa kura hapo kesho katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
mjini New York. Wakati huo huo Muhammad Swabih, Naibu Katibu Mkuu wa
Arab League anayeshughulikia masuala ya Palestina amesema kwamba, safari
ya Richard Falk mjini Cairo ni muhimu na kusisitizia udharura wa
kuungwa mkono mapendekezo na maazimio ya kimataifa kuhusiana na taifa la
Palestina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment