Mapigano makali yanaendelea
kuripotiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baina ya waasi
wa M23 na vikosi vya serikali. Mashuhuda wanasema, mapigano baina ya
pande mbili yanaendelea kushuhudiwa katika eneo la Kibumba lililoko
jirani na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda. Taarifa zaidi zinasema kuwa,
milio ya risasi imeendelea kusikika na kuzusha wasi wasi mkubwa huku
baadhi ya raia wakilazimika kuyakimbia makazi yao. Tayari Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Augustin Matata Ponyo ameutaka Umoja
wa Mataifa uwawekee vikwazo viongozi wa serikali ya Rwanda kutokana na
kuchochea machafuko mashariki mwa Kongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment