Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 13, 2012

Maandamano ya Wamisri dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel



Maandamano ya Wamisri dhidi ya utawala wa Kizayuni wa IsraelKwa mara nyingine tena Misri imeshuhudia mudhahara na maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wananchi wa nchi hiyo wameandamana kupiga nara za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina pamoja na harakati za utawala huo ghasibu dhidi ya nchi za Kiarabu. Kuonesha mfungamano na taifa la Palestina na kulaani mashambulio ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza ndio uliokuwa msukumo wa kufanyika maandamano hayo ya maelefu ya Wamisri katika mji mkuu Cairo.
Maandamnao hayo ya siku ya Jumatatu yalifanyika kwa wito wa maelfu ya asasi za kiraia na makundi ya kisiasa ya Misri. Wananchi wa Misri wametoa wito katika maandamano hayo wa kurejeshwa nyumbani balozi wa Misri huko Tel Aviv, kusimamishwa upelekwaji gesi Israel na kufunguliwa kikamilifu kivuko cha Rafah kwa ajili ya kupelekwa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina hususan wakazi wa Gaza.
Hisia dhidi ya Uzayuni zimeongezeka mno nchini Misri tangu kuangushwa kwa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak. Licha ya kuwa tangu kutiwa saini mkataba wa Camp David mwaka 1979 hakuna wakati ambao mtazamo wa wananchi wa Misri dhidi ya Uzayuni ulitetereka na kuingia dosari, lakini kuweko dikteta kama Hosni Mubarak ambaye alikuwa ngome ya siasa za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kulizuia kutangazwa wazi mtazamo wa wananchi hao dhidi ya Israel. Lakini kuibuka mazingira mapya nchini Misri na kufunguliwa ukurasa mpya wa anga ya kisiasa katika nchi hiyo kumewarahisishia Wamisri njia ya kubainisha wazi na dhahir shahir mitazamo yao kuhusiana na masuala mbalimbali likiweko suala la uhusiano wa nchi hiyo na tawala nyingine ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ni karibu miaka miwili sasa ambapo suala la kuangaliwa upya mkataba wa Camp David na hata kukatwa uhusiano wa kidiplomasia wa Cairo na Tel Aviv limegeuka na kuwa miongoni mwa matakwa makuu ya kitaifa nchini Misri. Hisia dhidi ya Wazayuni huko Misri zimeshtadi zaidi pia baada ya vikosi vya Israel kuwashambulia wanausalama wa Kimisri katika jangwa la Sinai lililoko katika mpaka wa nchi hiyo na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Nukta muhimu ya kuzingatia ni kuwa, kutokana na kuweko mafungano baina ya Wamisri na Wapalestina, hisia dhidi ya Uzayuni nchini Misri zimekuwa zikiongeza kadiri utawala huo ghasibu unavyoshadidisha mashambulio na jinai zake dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Katika hali ya hivi sasa, sio Wamisri tu, bali akthari ya vyama na makundi ya kisiasa ya nchi hiyo yanataka Cairo ikabiliane na utawala wa Tel Aviv. Wananchi wa Misri wanamtaka rais wa nchi hiyo Muhammad Mursi atazame upya mapatano yaliyofikiwa baina ya Cairo na Tel Aviv katika zama za tawala zilizotangulia nchini humo. Takwa hilo linatolewa katika hali ambayo, uhusiano wa Misri na Israel hivi sasa umefikia kiwango cha chini kabisa. Hii ina maana kwamba, kengele ya hatari kwa utawala wa Kizayuni imelia nchini Misri; sauti ambayo imesikiwa pia na viongozi wa Israel na ndio maana wakaingiwa na kiwewe kikubwa.

No comments:

Post a Comment