Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 2, 2012

DRC yatuhumiwa kwa kuwatesa wafungwa



DRC yatuhumiwa kwa kuwatesa wafungwa
Taasisi moja isiyo ya kiserikali ya kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeikosoa vikali serikali ya Kinshasa kwa kuwatesa wafungwa. Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo imeeleza kuwa, kuteswa wafungwa na mahabusu limekuwa jambo la kawaida kufanywa na polisi wa nchi hiyo. Taasisi hiyo inayoendeshwa kwa misaada ya Umoja wa Ulaya hadi sasa imeshafanya uchunguzi wake katika maeneo sita kati ya kumi na mbili ya nchi hiyo na kugundua kwamba, serikali ya Kongo imeshindwa kukabiliana na vitendo hivyo vya utesaji. Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Haki za Binadamu nchini Kongo amesema kuwa, kikosi cha usalama hulazimika kuwatesa watuhumiwa ili wakiri makosa wasiyoyafanya. Amesema kuwa, licha ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo kutia saini makubaliano ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya utesaji watu, lakini nchi hiyo bado haijatekeleza kivitendo makubaliano hayo na inaendeleza wimbi la kuwatesa wafungwa na mahabusu.

No comments:

Post a Comment