Kwa akali watu 22 wamepoteza maisha na wengine 111 kujeruhiwa,
baada ya kutokea mlipuko wa lori lililobeba gesi huko Riyadh, mji mkuu
wa Saudi Arabia. Taarifa zinasema kuwa, mlipuko huo umejiri baada ya
lori lililokuwa limebeba gesi kugonga daraja mashariki mwa Riyadh.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mlipuko huo pia ulisababisha magari mengine
saba kuteketea na kuleta maafa makubwa kwenye nyumba za jirani na tukio
hilo. Wakati huohuo, Fuad Ibrahim mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa
Saudi Arabia amesema kuwa, mapema leo asubuhi imetokea milipuko miwili
mmoja ukijiri kwenye makazi ya raia na mwengine katika kituo cha mafuta.
Ibrahim ameongeza kuwa, mlipuko huo umetokea kwenye bomba la mafuta, na
inahisiwa kwamba hiyo ni hujuma iliyotekelezwa na kundi maalumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment