Sheikh
Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba
cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi
Novemba 1, 2012. Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa
mara ya pili jana pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza
kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe
jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu na kuiba mali vyote vikiwa na
thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote
waliyakanusha. Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote
isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado
Mkurugenzi was Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia
dhamana kwa mshtakiwa namba moja. Ulinzi katika mahakama hiyo haujawahi
kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine,
palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma,
polisi wa kutuliza gharsia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na
mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo jirani na
mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam. Kikundi kidogo cha wafuasi wa
ssheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara
na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua
kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku polisi
wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya
barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika. Kwa mujibu
wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao
walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza
vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanbya
maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe. Kesi hiyo
iliahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena |
No comments:
Post a Comment