Habari kutoka Syria zinasema kuwa milipuko kadhaa
imetokea karibu na mji wa Damascus na kusababisha maafa na uharibifu
mkubwa. Habari zaidi zinasema kuwa, milipuko minne ya mabomu imesikika
kandokando mwa Damascus ukiwemo mji wa Jaramana yapata kilomita 10
kusini magharibi mwa Damascus. Televisheni ya Taifa ya Syria imeonyesha
picha za baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na milipuko hiyo na maafisa wa
usalama wamesema uchunguzi umeanza. Baadhi ya duru zimearifu kuwa ni
watu 34 waliouawa na duru zingine zimeripoti watu 40 ndio waliouawa.
Serikali imeyanyooshea kidole cha lawama makundi ya wapinzani wenye
silaha pamoja na mtandao wa kigaidi wa Al-qaeda ambao unawasaidia waasi
hao. Mashambilizi ya mabomu mjini Damascus si jambo geni na katika miezi
ya huko nyuma magenye ya watu wenye silaha yamekuwa yakitekeleza hujuma
kama hizo kwa msaada wa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani
pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabi kama vile Qatar na Saudi Arabia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment