Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, November 19, 2012

OIC yataka Wapalestina wa Gaza wasaidiwe haraka



OIC yataka Wapalestina wa Gaza wasaidiwe haraka Mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa yameingia siku ya 6 leo, huku idadi ya wananchi wa Palestina wanaouawa na kujeruhiwa ikizidi kuongozeka.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ametaka kupelekwa haraka misaada ya tiba katika Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo Naibu Waziri wa Tiba wa serikali halali ya Palestina ametahadharisha juu ya hatari zinazotokana na ukosefu wa dawa na vifaa vya tiba katika ukanda huo. Hassan Khalaf amesema, hali ya tiba na matibabu huko Gaza ni mbaya na kwamba ongezeko la majeruhi kutokana na mashambulizi ya Israel limesababisha ukosefu wa dawa na vifaa vya tiba. 
Wapalestina wasiopungua 96 wameuawa shahidi na wengine 900 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya siku 6 ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza.
Wakati huo huo msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amelaani mashambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutaka mashambulizi hayo yasitishwe mara moja. Vilevile walimwengu wameendelea kuandamana katika kona mbalimbali duniani kulaani na kupinga mashambulizi hayo ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

No comments:

Post a Comment