Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran amesema kuwa, kustawishwa mahusiano na nchi huru na zile
zisizofungamana na siasa za upande wowote, ni miongoni mwa malengo makuu
ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Akizungumza na Mshauri wa Rais wa Ghana
mjini Tehran Saeed Jalili ameitaja nafasi muhimu ya Ghana katika
kuundwa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM na
kukosoa misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi katika
kuamiliana na kadhia kama vile haki za binadamu, ugaidi na kuizuia Iran
isitumie nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.
Jalili ameongeza kuwa, ulimwengu wa leo unahitajia ubunifu wenye shabaha ya kuleta mabadiliko katika mambo yasiyokuwa ya kiadilifu yanayotawala leo hii katika uga wa kimataifa. Kwenye mazungumzo hayo, naye Mshauri wa Rais wa Ghana amesema kuwa, kuna ulazima wa kuimarishwa mashirikiano kati ya Accra na Tehran, na kuelezea matumaini yake kwamba jumuiya ya NAM chini ya uenyekiti wa Iran inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kushughulikia masuala mbalimbali tata yanayojiri hivi sasa ulimwenguni.

No comments:
Post a Comment