Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) nchini
Tanzania, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ameanza kutafuta suluhu kati ya
viongozi wa dini za Kislamu na Kikristo ili kuweka misingi ya waumini
wote kuheshimania na kudumisha amani nchini.
Prof. Lipumba amesema atafanya jitihada za kukutana na
viongozi wa Kiislamu na Kikrito pamoja na wanasiasa akiwemo Rais Jakaya
Kikwete ili kufikia lengo lake. Kiongozi huyo ameongeza kwamba,
serikali
ikitumia busara na kuwasiliana na Maimamu wa misikiti pamoja na
viongozi wa Kikristo panaweza kupatikana natija. Lipumba amewaomba
Waislamu wasishiriki kwenye maandamano baada ya Sala ya Ijumaa kwa kuwa
hali hiyo ya mtafaruku ndiyo inayochochea ghasia na dhana kwamba
Tanzania imetumbukia katika machafuko ya kidini.
Wiki iliyopita viongozi wa makundi mbalimbali ya waumini wa
Kiislamu pamoja na polisi, walikuwa wakihimiza waumini kutojihusisha na
maandamano hayo waliyoyaita haramu kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa
amani. Waislamu wamekuwa wakiandamana wakitaka kuachiliwa huu Katibu wa
Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye
anaendelea kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi.
No comments:
Post a Comment