Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 2, 2012

Mgombea wa urais Marekani atiwa mbaroni

Mgombea wa urais Marekani atiwa mbaroni
Duru za habari nchini Marekani zinaarifu kuwa, Jill Stein mgombea wa urais wa Novemba sita mwaka huu kwa tiketi ya chama cha Kijani cha Green Party, ametiwa mbaroni na maafisa wa usalama kwa tuhuma za kupinga kupitishwa bomba la Keystone XL katika jimbo la Texas nchini humo. Wanaharakati wanaopinga upitishwaji wa bomba hilo, wameelezea kuwa, Jill aliachiliwa baada ya kushikiliwa kwa masaa kadhaa katika jela ya Wiwid nchini
humo. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, upinzani wa kupinga bomba la Keystone XL ulianza tangu mwezi mmoja uliopita. Mtandao wa mgombea huyo Jill Stein umeandika kuwa, alikamatwa wakati alipokuwa amekwenda eneo la upinzani kwa ajili ya kutaka kuzungumzia masuala muhimu kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa Marekani imekuwa ikizikosoa nchi nyengine duniani kwa kukiuka demokrasia na haki za binaadamu, wakati yenyewe ndio mtendaji mkubwa wa vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment