Kamanda
wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus
Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo
zilikutwa kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni
majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha
leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu
kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali .
(Picha na Mahmoud Ahmad Arusha)
MNAMO TAREHE 22/11/2012 MUDA WA
SAA 3:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA OLMATEJOO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA,
WATU WATATU (AMBAO MAJINA YAO BADO HAYAJATAMBULIKA) WANAOSADIKIWA
KUWA NI MAJAMBAZI WALIUAWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA
WAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI.
TUKIO HILO
LILITOKEA MARA BAADA YA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KUPATA TAARIFA
KUTOKA KWA RAIA WEMA AMBAO WALIELEZA KWAMBA, KATIKA ENEO HILO KULIKUWA
NA WATU WATANO AMBAO WANAWATILIA SHAKA, NDIPO BAADHI YA ASKARI
WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA KUFANYA UCHUNGUZI.
MARA BAADA YA ASKARI HAO KUFIKA
ENEO HILO, WATU HAO WALISHTUKA NA MMOJA WAO ALIYEKUWA NA SILAHA AINA YA
BASTOLA KIUNONI ALIITOA NA KUANZA KUWAFYATULIA RISASI ASKARI HAO.
KUTOKANA NA HALI HIYO ASKARI HAO WALIAMUA KUJIBU MAPIGO NA KUFANIKIWA
KUWAJERUHI WATU WATATU KATI YA WATANO NA WENGINE WAWILI WALIFANIKIWA
KUKIMBIA PAMOJA NA BASTOLA.
WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA
NJIANI WANAPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA AJILI YA MATIBABU.
ASKARI HAO WALIFANIKIWA KUPATA BEGI LILILOTUPWA NA WATU HAO NA MARA
BAADA YA KUPEKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI; MOJA AINA YA SHORTGUN NA
NYINGINE AINA YA RIFLE YENYE NO. 08805 AMBAYO ILIKUWA IMEKATWA MTUTU
PAMOJA NA KITAKO.
MBALI NA BUNDUKI HIZO PIA
WALIKUTWA NA RISASI 16 ZA SHORTGUN, KITAKO NA MTUTU WA BUNDUKI AINA YA
RIFLE, MTALIMBO (KIPANDE CHA CHUMA) AMBACHO KINASADIKIWA KUWA KINATUMIWA
KATIKA SHUGHULI ZA UVUNJAJI, RUNGU MOJA, PANGA MOJA, TUPA TATU ZA
KUNOLEA PANGA, SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) AMBAZO NI
SURUALI MOJA, T-SHIRT MOJA NA KOFIA MOJA. PIA ZILIPATIKANA KOFIA MBILI
ZINAZOTUMIKA KUFICHA USO PAMOJA NA KITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA,
LESENI YA UDEREVA NA KITAMBULISHO CHA MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI
DODOMA.
MPAKA HIVI SASA JESHI LA POLISI
MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWATAFUTA WATU WAWILI AMBAO WALIKIMBIA NA PIA
LINAFANYA JITIHADA ZA KUWATAMBUA WATU WALIOUAWA AMBAPO MPAKA HIVI SASA
MIILI YAO IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU. ASANTENI KWA
KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) LIBERATUS SABAS
TAREHE 22/11/2012.
No comments:
Post a Comment