Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, November 19, 2012

Pinda awataka Watanzania kuishi kwa amani



Pinda awataka Watanzania kuishi kwa amani
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kuishi kwa amani na kuweka kando tofauti zao za kidini ili nchi isonge mbele.
Akizungumza wakati wa kuzindua Taasisi ya Kiarabu Tanzania jijini Dar es Salaam, Pinda amesema Watanzania wameishi kama ndugu kwa muda mrefu bila ya kujali itikadi zao za kidini na ametaka jambo hilo liendelee kuwepo. Amesema machafuko yaliyoshuhudiwa majuzi Tanzania bara na Visiwani Zanzibar ambapo viongozi wa Kiislamu walikamatwa na vilevile makanisa kuchomwa yanatishia historia ndefu ya umoja na mshikamani miongoni mwa Watanzania wa dini mbalimbali.
Wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo, Pinda alikutana na baadhi ya Mashekhe wa Dar es Salaam na kuwaahidi kwamba kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda itaendeshwa kwa uadilifu.

No comments:

Post a Comment