Habari kutoka Guelmim kusini mwa Morocco zinasema kuwa, helikopta
moja ya kijeshi imeanguka katika eneo hilo na kusababisha vifo vya
wanajeshi 9. Habari zaidi zinasema wanajeshi wengine 2 wamejeruhiwa
vibaya na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za karibu na eneo
hilo. Wizara ya Ulinzi ya Morocco imesema huenda hali mbaya ya hewa
ndiyo iliyosababisha ajali hiyo ingawa uchunguzi umeanzishwa kubaini
chanzo chake. Mwaka uliopita takribani wanajeshi 80 walipoteza maisha
yao katika eneo hilo la Guelmim katika ajali mbaya ya ndege. Morocco
ina kambi kubwa ya jeshi la wanaanga katika eneo hilo la kusini mwa nchi
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment