Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, November 18, 2012

OIC: Mauaji ya Waislamu wa Myanmar ni ya Kimbari


OIC: Mauaji ya Waislamu wa Myanmar ni ya Kimbari
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC wamemaliza mkutano wao wa siku tatu nchini Djibouti leo Jumamosi ambapo wito umetolewa wa kuchukuliwa hatua za dharura kukomesha mauaji ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar. Mkutano huo ulioanza siku ya Alhamisi umejadili kwa kina mashambulizi ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa ya mwisho ya mkutano huo sambamba na kulaani jinai za Wazayuni huko Gaza, imezitaka nchi wanachama kuchukua hatua za kivitendo kukomesha jinai hizo. Pia wajumbe wamekubaliana kwamba OIC ipewe nafasi zaidi ya kushughulikia kadhia ya Syria. Jumuiya hiyo imepinga uingiliaji wowote wa kigeni katika mgogoro wa Syria na kusisitiza kwamba Wasyria wenyewe ndio watakaoweza kutatua mgogoro wao bila kushinikizwa na madola ya kigeni.

No comments:

Post a Comment