Waasi wa Syria ambao wanaungwa mkono na nchi za Magharibi na hasa
Marekani na zile za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na Uturuki
wameendeleza jinai zao kwa kuushambulia kwa makombora msikiti mmoja
ulioko katika mji wa Halab nchini humo. Picha ya mkanda wa video
iliyotolewa hivi karibuni inawaonyesha wapiganaji hao wa kundi la waasi
wakitenda jinai hiyo na baada ya kuuangamiza kikamilifu msikiti huo
wakaanza kushangilia na kucheza dansi kwenye mabaki ya msikiti huo.
Kundi hilo la waasi limefanya jinai kadhaa nchini humo ikiwa ni pamoja
na kuwafyatulia risasi wanajeshi wa serikali baada ya kuwa
wameshawakamata na kuwafunga kamba miguuni na mikononi. Waasi
walianzisha machafuko nchini humo mwezi Machi 2011, kwa shabaha ya
kuiondoa madarakani serikali halali na iliyochaguliwa na wananchi ya
Rais Bashar Assad wa Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment