Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, makundi yanayobeba silaha
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamewaua karibu watu 300
wakiwemo watoto 83 kati ya mwezi Aprili na Septemba mwaka huu kinyume
cha sheria katika jimbo la Kivu Kaskazini. Navanethem "Navi" Pillay Mkuu
wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa,
makundi hayo yamefanya zaidi ya mashambulio 75 kwenye vijiji mbalimbali
vya jimbo hilo lililogubikwa na machafuko na kuwaua watu 264 wakiwemo
watoto 83. Pillay ameongeza kuwa, kumeshuhudiwa vitendo vya ukiukaji
haki za binadamu na mauaji ya makumi ya wananchi wa eneo hilo katika
miezi ya hivi karibuni. Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya
Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Kongo kuchukua hatua za haraka za
kuwalinda raia wa eneo hilo na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika
wote ili kuzuia kuendelezwa jinai katika eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment