Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 27, 2012

Kiongozi Mkuu: Iran imefanikiwa katika malengo yake


Kiongozi Mkuu: Iran imefanikiwa katika malengo yake Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amekutana na makamada wa jeshi la majini la Iran na kusisitiza juu ya nafasi muhimu ya jeshi hilo katika kulinda amani na usalama wa Ghuba ya Uajemi.
Ayatullah Khamenei ambaye amekutana na makamanda hao wa jeshi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Majini, ameashiria malengo ya muda mrefu ya Jamhuri ya Kiislamu na mafanikio mtawalia ya utawala wa Kiislamu hapa nchini katika kufikia malengo yake na akasema kuwa, hali ya mambo katika eneo la Mashariki ya Kati na katika uga wa kimataifa inaonesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu imepata mafanikio makubwa.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa moja ya sababu za makelele ya kipropaganda yanayofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mafanikio hayo na kuongeza kuwa: Tunapofanya ulinganisho kati ya siasa za Mashariki ya Kati za nchi za Magharibi na siasa za Jamhuri ya Kiislamu kuhusu eneo hilo tutaona kuwa siasa za Iran zimekaribia zaidi kwenye malengo yake.
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran amesema pwani kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan pwani ya Bahari ya Oman ni utajiri mkubwa wa kitaifa. Ameongeza kuwa iwapo viongozi wa serikali na asasi nyingine hapa nchini watayatazama maeneo ya baharini kwa mtazamo wa kistratijia basi maeneo hayo muhimu yanaweza kuwa sababu ya nguvu na uwezo mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu.

No comments:

Post a Comment