Kamanda mmoja wa wapiganaji wa kundi la Boko Haram ameuawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la serikali ya Nigeria.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Nigeria imesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kumuua Ibn Saleh Ibrahim aliyekuwa mmoja wa makamanda wa kundi la Boko Haram katika shambulizi lililofanyika kwenye mji wa Maiduguri. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa watu wengine kadhaa waliokuwa pamoja na Bin Saleh Ibrahim pia wameuawa katika operesheni hiyo.
Jeshi la Nigeria limesema kuwa Saleh Ibrahim alihusika na mauaji ya jenerali mstaafu Mamman Shuwa ambaye alikuwa mmoja wa mashujaa wa vita vya ndani nchini Nigeria katika miaka ya 60. Kiwango kikubwa cha silaha pia kimekamatwa katika operesheni hiyo.
Kundi la Boko Haram linahusika na machafuko ya sasa ya Nigeria hususan katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyo na limetuhumiwa kuhusika na mauaji ya mamia ya watu tangu mwezi Julai mwaka 2009.

No comments:
Post a Comment