Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, November 14, 2012

Kiongozi Muadhamu akosoa uhuru wa Kimagharibi



Kiongozi Muadhamu akosoa uhuru wa KimagharibiKiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amekosoa mfumo wa uhuru wa Kimagharibi ambao umepelekea kuibuka ubaguzi, utumizi mabavu na sera za kivita.
Ayatullah Khamenei amefafanua zaidi kuhusu kesi za uhuru wa Kimagharibi na kusema kwa mfano 'uhuru wa kiuchumi' huko Magharibi unapelekea kuibuka mfumo unaowapa faida watu wachache. Pia ameashiria 'uhuru wa kisiasa' katika nchi za Magharibi' ambao umepelekea kuhodhiwa madaraka na makundi mawili ya kisiasa. Halikadhalika ameashiria 'uhuru katika masuala ya kimaadili' huko Magharibi jambo ambalo limepelekea kudhihiri ufisadi wa kimagharibi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo mjini Tehran katika mkutano na wasomi, wanazuoni na watafiti. Ayatullah Khamenei amekosoa fikra zinazosema kuwa uhuru ni kutokuwepo vizingiti hata kidogo. Kiongozi Muadhamu ameashiria tofauti za mitazamo kati ya Uislamu na Magharibi na kusema, tofauti katika mtazamo wa Kiislamu na Kimagharibi uko katika msingi wa uhuru. Kiongozi Muadhamu amesema katika mfumo wa kifikra wa kiliberali, uhuru uko katika msingi wa Humanism wakati ambapo katika Uislamu imani kwa Mwenyezi Mungu na kupinga shirki ndio msingi wa uhuru. Aidha amesema, heshima ya mwanaadamu ni moja ya misingi ya uhuru katika Uislamu.

No comments:

Post a Comment