Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, July 24, 2013

Mufti wa Syria asisitiza kudumishwa amani na udugu


Mufti wa Syria asisitiza kudumishwa amani na udugu
Mufti wa Syria ametaka kudumishwa amani, mapenzi, udugu na utulivu nchini humo na kote ulimwenguni. Sheikh Ahmad Badruddin Hassun  ameashiria jinsi dini tukufu ya Kiislamu inavyosisitizia sana umuhimu wa kudumishwa amani na mapenzi baina ya watu na jinsi Mtume wa Uislamu (SAW) alivyolitia mkazo sana jambo hilo na amelaani vikali jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi huko Syria ikiwemo kuwaua ovyo raia kuharibu miji ya nchi hiyo.
Sheikh Ahmad Badruddin Hasun aidha amesema, magaidi wameshindwa huko Syria na kwamba mafanikio ya jeshi la nchi hiyo katika kuyaangamiza makundi ya kigaidi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ni dhihirisho tosha kuwa siku za mwisho za magaidi hao zimekaribia. Sheikh Hasun amesema, njama za miaka miwili iliyopita za nchi za Magharibi na vibaraka wao wa Kiarabu katika eneo la Mashariki ya Kati za kutaka kuilazimisha serikali ya Damascus isalimu amri mbele ya matakwa yao  zimegonga ukuta na kwamba nchi hizo sasa zinajaribu kila ziwezalo ili kujipapatua kutoka kwenye kinamasi zilichokwamba ndani yake huko Syria.

No comments:

Post a Comment