skip to main |
skip to sidebar
M23 waibua wasi wasi mashariki mwa Kongo
Mwanaharakati mmoja wa kutetea haki za binadamu amesema kuwa,
waasi wa M23 wanazitishia familia za wahanga ambao walioko kwenye mpaka
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda wasitoe taarifa zozote
zilizokuwa dhidi yao kwa shirika la kutetea haki za binadamu la Human
Rights Watch. Mwanaharakati huyo ambayo hakuwa tayari kujitambulisha
wasifa wake amesema kuwa, waasi wa M23 wamekuwa wakizituhumu familia za
wahanga kwa kutoa taarifa zao kwa shirika hilo la kutetea haki za
binadamu. Shirika la Human Rights Watch hivi karibuni lilitoa taarifa na
kueleza kuwa, waasi wa M23 walioko mashariki mwa Kongo waliwahukumu
adhabu ya kifo watu 44 bila ya kuwafungulia mashtaka katika jimbo la
Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo, kwa makosa ya kuwabaka wanawake na
wasichana 61 na kuwafanyisha kazi kwa nguvu watoto wadogo. Wakati
huohuo, waasi wa M23 wanawashikilia vijana wasiopungua 50 kwa tuhuma za
kushiriki kwenye maandamano yaliyopelekea kuchomwa moto maduka ya watu
wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda huko mashariki mwa Kongo. Hayo
yameelezwa na Luteni Kanali Vianney Kazarama Msemaji wa kundi la waasi
wa M23.
No comments:
Post a Comment