Marekani imeitaka Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi wa Machi 23
huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Washington imesema,
kuna ushahidi kwamba maafisa wa jeshi la Rwanda wanawasaidia waasi wa
M23. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na Washington kufuatia mapigano
yaliyojiri hivi karibuni kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali ya
Kinshasa karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi huko
mashariki mwa Kongo na ni eneo tajiri kwa madini. Jen Psaki, msemaji wa
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amesema, Washington inaitaka
Rwanda iache mara moja kuwaunga mkono waasi wa Machi 23 na kuondoa
vikosi vyake huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wito
huo umetolewa ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya John Kerry, Waziri wa
Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuwa mwenyekiti wa kikao maalumu cha
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kitakachojadili eneo la maziwa
makuu ya Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment