Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, August 19, 2013

Wapinga mapinduzi Misri kuendelea kuandamana


Wapinga  mapinduzi Misri  kuendelea kuandamana
Muungano wa wapinga mapinduzi ya kijeshi nchini Misri umeapa kuendelea na maandamano licha ya vikosi vya usalama kuendeleza ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Mursi. Hii leo pia wafuasi wa Mursi wameendelea kuandamana katika mji mkuu Cairo na miji mingineyo ya nchi hiyo wakitaka kiongozi huyo aliyepinduliwa na jeshi arejeshwe madarakani. Wakati huo huo wafuasi wa Mursi wametaka kufanyike uchunguzi rasmi wa mauaji ya waandamani 36 waliokuwa wanashikiliwa na polisi yaliyotokea jana walipokuwa wakisafirishwa na gari la polisi.
 Katika upande mwingine Umoja wa Ulaya umesema kwamba, iwapo umwagaji damu haitositishwa nchini Misri , katika siku zijazo itaangalia uhusiano wake na jeshi la nchi hiyo na serikali ya mpito ya Cairo.   Hata hivyo Nabil Fahmy Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ametetea ukandamizaji mkubwa wa jeshi dhidi ya wafuasi wa Mursi huku Mkuu wa Jeshi Jenarali Abdul Fattah al Sisi akisisitiza kwamba hawatoacha kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni ghasia na machafuko.

No comments:

Post a Comment