Umoja wa Mataifa umeanza kupeleka misaada ya kibinadamu kwa raia
walioathiriwa mafuriko nchini Sudan. Mashirika ya misaada ya kibinadamu
inayofungamana na Umoja wa Mataifa yameanza zoezi la upelekaji misaada
hiyo kwa raia takribani laki moja na nusu waliokumbwa na mafuriko katika
viunga vya mji mkuu Khartoum. Kifurushi cha awali cha misaada hiyo ya
kibinadamu kinajumuisha chakula na maji safi ya kunywa. Raia hao
wameathiriwa na mafuriko hayo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha nchini Sudan tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Agosti. Ripoti za
utabiri wa hali ya hewa zinaonesha kuwa, mafuriko na mvua kali
zitaendelea kunyesha katika siku kadhaa zijazo nchini Sudan na kuathiri
idadi kubwa zaidi ya watu. Njia na barabara nyingi za mji wa Khartoum
hazipitiki kutokana na kusambaa maji kila mahala huku sehemu kubwa ya
mji mkuu huo ikiwa haina huduma ya maji na umeme kutokana na kuharibika
miundo mbinu ya huduma hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment