Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, August 16, 2013

SHEIKH PONDA APELEKWA GEREZANI SEGEREA


Wakili wa Sheikh Ponda

DAR ES SALAAM, Tanzania

Wakili wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Ponda aliyekuwa  amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI)  alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumwamishia katika gereza la Segerea.

Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kimenisikitisha na kunishitua sana ….ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni’alisema wakili Jumaa.

Agosti 14 mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamia katika wodi hiyo ya MOI na wakili wa serikali Tumaini Kweka alimsomea shitaka Ponda ambaye anakabiliwa na kesi hiyo ya Jinai Na.144 ya mwaka huu.
 
CHANZO:HABARI MSETO BLOG

No comments:

Post a Comment