Martin Kobler amesema maeneo ya raia na vituo vya jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO vimeshambuliwa na kwamba amelitaka jeshi hilo kuchukua hatua za dharura za kuwalinda raia na kuzuia kusonga mbele wapiganaji wa kundi la M23.
Duru za habari zinasema kuwa makombora matatu yamelenga mji wa Goma na kuua watu kadhaa wakiwemo watoto wadogo mawili. Vilevile habari zinasema kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 Alkhamisi ya jana waliingia katika ukanda wa usalama unaozunguka mji wa Goma huko mashariki mwa Congo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda. Maafisa wa serikali ya Congo wanasema kundi la M23 limevurumisha makombora kadhaa katika mji wa Goma na kwamba makombora mengine yamevuka mpaka na kuingia katika ardhi ya Rwanda.
Serikali ya Kigali imelaani tukio hilo na kulilaumu jeshi la serikali ya Kinshasa kwa shambulizi hilo. Wizara ya Ulinzi ya Rwanda imesema shambulizi hilo haliwezi kuhalalishwa kwa njia yoyote ile.
No comments:
Post a Comment