Chama tawala cha Kongresi
ya Taifa Sudan kimefichua kuwepo njama za mashirika ya kijasusi ya
Marekani na Utawala wa Kizayuni ya Israel za kuwaunga mkono waasi nchini
Sudan lengo likiwa ni kuyakalia kwa mabavu maeneo yenye utajiri wa
mafuta nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la
Habari la Fars, chama hicho tawala nchini Sudan kimesema majasusi wa
Israel na Marekani wanaunga mkono makundi ya waasi hasa kundi la JEM la
Darfur. Chama cha Kongresi ya Taifa kimesema pamoja na kuwepo oparesheni
hizo za majasusi wa Kizayuni na Marekani,
jeshi la Sudan liko macho na
litaangamiza njama hizo kikamilifu. Aidha chama hicho kimesema Umoja wa
Mataifa umeshatoa ripoti inayoonyesha kuwa serikali ya Sudan Kusini
inawaunga mkono waasi wanaoipinga serikali ya Sudan. Hamid Sadiq wa
Kongresi ya Taifa amesema ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imethibitisha
ukweli ambao Sudan imekuwa ikiusema mara kwa mara. Wiki iliyopita pia
Qutbi al Mahdi mmoja wa viongozi wa chama tawala cha Kongresi ya Taifa
ya Sudan alifichua njama za nchi za Magharibi za kutaka kuwalazimisha
watu wa Sudan wawe Wakristo sambamba na kuibua hitilafu za kikabila
nchini humo lengo likuwa ni kuipokonya nchi hiyo utambulisho wake asili.
No comments:
Post a Comment