Shirika la Msalaba Mwekundu limetangaza kuwa, zaidi ya watu 60
wamejeruhiwa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya jeshi la Sudan
Kusini na kundi moja la waasi nchini humo. Shirika hilo limeongeza kuwa,
katika kipindi cha wiki mbili zilizopita karibu watu 62 waliojeruhiwa
katika apigano hayo walitibiwa katika kituo kimoja cha afya cha shirika
hilo na kwamba. Mmoja wa viongozi wandamizi wa shirika hilo amenukuliwa
akisema kuwa, idadi rasmi ya maafa yaliyotokana na machafuko hayo ya
pande mbili haijafahamika kutokana na kwamba, hadi sasa hakuna taasisi
yoyote iliyofika eneo la tukio na kufanya uchunguzi. Ameongeza kuwa,
kutokana na viongozi wa Juba kukosa ripoti kamili ya mapigano hayo,
idadi ya wahanga inaweza kupindukia ile iliyotajwa hapo awali. Hivi
karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini,
alielezea kusikitishwa kwake na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na
Jeshi la Sudan Kusini dhidi ya waasi wanaoongozwa na David Yauyauambao
wanaipinga serikali ya Juba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment