Zaidi ya watu milioni 12 wametaka iondoshwe marufuku ya hijabu
nchini Uturuki. Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi Serikalini nchini
Uturuki amesema kuwa, jumla ya watu milioni 12 wanapinga kuendelezwa
marufuku ya hijabu mashuleni na hata kunyimwa ajira wanawake wanaovaa
hijabu kwenye sekta za serikali nchini humo. Mkuu wa Vyama vya
Wafanyakazi Serikalini nchini Uturuki amewasilisha ombi hilo kwa Waziri
wa Kazi na Ustawi wa Jamii wa Uturuki jumla ya saini za watu milioni 12
wanaotaka kuondoshwa marufuku ya hijabu nchini humo. Waziri wa Kazi na
Ustawi wa Jamii wa Uturuki ameahidi kulipeleka ombi hilo mbele ya kikao
cha baraza la mawaziri nchini humo ili lijadiliwe upya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment