Matokeo yasiyo rasmi ya kura ya maoni ya katiba mpya nchini
Zimbabwe, yanaonyesha kwamba, wananchi wameipigia kura ya ndio katiba
hiyo ambayo inapunguza madaraka ya rais wa baadaye wa nchi hiyo. Ripoti
zilizosambazwa leo kutoka vituo vya kuhesabu kura, zinaonyesha kuwa,
watu milioni tatu na laki moja kati ya watu milioni tatu na laki nne
waliofika kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo, wameipigia kura ya
ndio katiba mpya ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inayokabiliwa na
mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Gazeti la Herald limeripoti kuwa, watu laki
mbili wameipigia kura ya hapana katiba hiyo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi
za nchi hiyo, Wazimbabwe milioni sita pekee ndio waliokamilisha
masharti ya kupiga kura nchini. Ilitarajiwa kuwa, hadi kufikia jioni ya
leo, Tume ya Uchaguzi nchini humo ingekuwa imekamilisha kazi za kuhesabu
kura na kutangaza matokeo rasmi ya kura hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment