skip to main |
skip to sidebar
Boko Haram yaua 19 kaskazini mashariki mwa Nigeria
Watu wasiopungua 19 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na
wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Hayo yameelezwa na wenyeji na watu walionusurika na nmashambulizi hayo.
Hadi sasa miili 19 imegunduliwa katika eneo palipojiri mashambulizi hayo
ya Boko Haram. Habari zinasema kuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram
walifunga barabara kuu karibu na mji wa Logumani umbali wa kilomita 30
kutoka katika mpaka wa Nigeria na Cameroon na kuanza kuua raia na
kuchoma moto malori matatu. Wahanga watano ambao miongoni mwao walikuwa
ni madereva wawili wa malori na wasaidizi wao waliuliwa kwa kupigwa
risasi na waliosalia walichinjwa. Boko Haram imetekeleza mashambulizi
hayo jana katika hali ambayo tarehe sita mwezi huu pia kundi hilo
liliushambulia msikiti mmoja huko Damboa katika jimbo la Borno na
kuwauwa waumini watano waliokuwa katika sala ya asubuhi.