Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, October 30, 2013

Israel yawaachia huru mateka 26 wa Palestina


Israel yawaachia huru mateka 26 wa PalestinaUtawala wa Kizayuni wa Israel umewaachilia huru mateka 26 wa Palestina, kama sehemu ya makubaliano ya kuanza tena mazungumzo eti ya amani  ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Sivan Weizman msemaji wa jela za Israel ameeleza kuwa, 21 kati ya mateka hao walioachiliwa huru ni wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na watano kati yao wanatoka Ukanda wa Gaza. Mateka 104 wa Palestina wanatarajiwa kuachiliwa huru  miezi ijayo kutoka katika jela za kuogofya za utawala ghasibu wa Israel.
Nderemo na vifijo vilizikika kuanzia leo asubuhi wakati familia na viongozi wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza walipokuwa wakiwapokea mateka hao walioachiliwa huru na Israel.
Hata hivyo mazungumzo hayo eti ya  kusaka amani kati ya Tel Aviv na Mamlaka ya Ndani ya Palestina yanapingwa na wananchi wengi na makundi ya mapambano ya Palestina.