Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, October 12, 2013

AU kuongeza askari wa AMISOM nchini Somalia


AU kuongeza askari wa AMISOM nchini SomaliaUmoja wa Afrika unapanga mikakati ya kuongeza idadi ya askari wa kulinda amani nchini Somalia AMISOM, kwa shabaha ya kupambana na wanamgambo wa kundi la al Shabab nchini humo. Tokea mwaka 2007, kikosi cha AMISOM  kiko nchini Somalia, na katika miaka miwili ya hivi karibuni kimefanya operesheni kadhaa  dhidi ya wanamgambo wa kundi hilo. Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetangaza kuwa wataongezwa askari 6,235 na kuifanya idadi ya wanajeshi walioko nchini humo kufikia elfu ishirini na tatu mia tisa na sitini na sita.
Hata hivyo uamuzi huo unapaswa kuthibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Imeelezwa kuwa gharama za kuendesha operesheni za AMISON zinadhaminiwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na wanajeshi wengi wa kikosi hicho wanatoka nchi za Uganda, Burundi na Kenya. Kundi la al Shabab limeshadidisha operesheni zake dhidi ya majeshi ya kigeni na hasa baada ya kupoteza udhibiti wa ngome zake hasa hasa katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.