IDADI ya miili iliyopatikana katika ajali ya meli ya
Mv. Skagit imezidi kuongezeka baada ya jana kupatikana miili 16 katika
maeneo ya Zanzibar na Bagamoyo Tanzania Bara. Kwa mujibu wa waziri wa
nchi ofisi ya rais makamo pili wa rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohammed
amesema maiti hao wamezikwa haraka haraka kutokana na kuharibika vibaya
pamoja na kwamba waliopatikana Bagamoyo wameshazikwa huko huko.
“Ni kweli maiti zimeongezeka leo mchana na baada ya
kuopolewa na zikikimbizwa haraka kuzikwa kwa sababu miili yenyewe tayari
imeshaharibika” alisema Aboud.
Aboud alisema kati ya maiti 16 zilizoptikana leo
maiti 5 zimepatikana huko Bagamoyo ambapo matayarisho ya mazishi yao
yamefanywa na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ya mkoa huo.
Maiti hizo zimekwenda kuzikwa katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mazishi huko Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Alisema idadi hiyo inafikisha maiti zilizopatikana
tangu kutokea kwa ajali hiyo jumatano iliyopita kufikia 94 ambapo idadi
kubwa ya waliofariki ni wanawake na watoto.
Bado watu 50 kati ya 290 waliokuwemo katika Mv.
Skagit hawajaonekana hadi hii leo na 146 wamepatikana wakiwa hai na
kupatiwa matibabu huku wengine wakiruhusiwa kurudi majumbani.
Akizungumza waandishi wa habari mmoja wa waokoaji
amesema wamepata miili hiyo ambayo yote ni ya watu wazima lakini wengi
wao wakiwa wanawake kuliko wanaume.
Alisema miili hiyo haiwezi kutambulika kwa kuwa
imeharibika vibaya lakini pia imeanza kutafunwa na samaki na baadhi yao
imeganda kaa mwilini mwao.
“Miili tunayoiopoa hivi sasa haiwezi kujulikana sura
kwa sababu haioneshi kabisa imeharibika vibaya sana lakini tunatambua
kuwa huyu ni mwanamke na mwanamme kutokana na nguo walizovaa tu lakini
kwa sura huwezi kumtambua” alisema muokoaji huyo.
Aidha alisema wanafanya kazi ya kujitolea ya ukozi
lakini katika katika mazingira magumu kutokan ana kukosa vifaa lakini
pia kuhofia maisha yao kutokana na kuwa hawana vitendea kazi vya
uhakika.
Operesheni ya uokozi inafanywa na vikosi vya ulinzi
na usalama vya serikali na wananchi wa kawaida wanaojitolea ambapo idadi
kubwa inayookoa miili hiyo kwa sasa ni wavuvi wwanaotoa taarifa kwa
vyomvo vinavyohusika na kisha waokoaji kufuata miiili hiyo ilipo na
kwenda kuichukua.
No comments:
Post a Comment