Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, December 28, 2014

MISRI NA MOROCCO ZAPIGA MARUFUKU FILAMU INAYOMUONESHA MUNGU

Misri na Morocco zimepiga marufuku filamu iliyotengenezwa Hollywood isioneshwe katika mataifa hayo ya Afrika Kaskazini. Vyombo vya habari nchini Morocco vimetangaza kuwa mameneja wa sinema katika pembe zote za nchi hiyo wamepewa maagizo ya kutoonesha filamu iliyojaa utata ya “Exodus: Gods and Kings,” kwa sababu “inamuonesha Mungu,” jambo ambalo ni haramu katika Uislamu. Mapema waziri wa utamaduni wa Misri, Gaber Asfour alisema kuwa filamu hiyo imejaa makosa lukuki ikiwa ni pamoja na madai kwamba “[Nabii] Mussa na Wayahudi ndio waliojenga mapiramidi,” na kuongeza kuwa, “hilo linapingana kabisa na taaarifa za kihistoria zilizothibitishwa”. Adiha, waziri huyo ameashiria kuwa filamu hiyo iliyoongozwa na Ridley Scott, ni ya kizayuni na imetengenezwa kwa malengo ya kisiasa. “Inatoa historia kwa mujibu wa uzayuni na ina makosa lukuki ya kihistoria na ndio maana tumeamua kuipiga marufuku”, alisema. Mapema mwezi Mei, mwandishi na mtunzi maarufu wa filamu Art Olivier alisema kuwa makampuni mengi ya filamu za Hollywood zinamilikiwa na wafanyabishara wa Kizayuni. Kwa miaka kadhaa Hollywood imekuwa ikitengeneza filamu nyingi zinazolenga kuuchafua Uislamu na Waislamu.

No comments:

Post a Comment