skip to main |
skip to sidebar
Shambulio la Taliban laua wa 44 Afghanistan
Wanamgambo waasi waliokuwa wamevalia sare za jeshi la taifa la
Afghanistan wameua watu 44 na kuwajeruhi wengine 100 baada ya kufanya
shambulio dhidi ya majengo ya serikali katika jimbo la Farah. Gavana wa
Jimbo la Farah Mohammad Akram Ekhpelwak amesema kuwa, kwa uchache
washambuliaji wanane waliuawa kwenye shambulio hilo. Amesema kuwa,
shambulio hilo lililofanywa na kundi la wanamgambo wa Taleban lilikuwa
na lengo la kuwakomboa wapiganaji wenzao waliokuwa wamefikishwa
mahakamani. Amesema kuwa, raia 34, wanajeshi sita na askari wanne
wameuawa kwenye shambulio hilo. Ekhpelwak ameongeza kuwa, shambulio hilo
lililenga majengo ya serikali zikiwemo ofisi ya mahakama na ile ya
Mwanasheria Mkuu.
No comments:
Post a Comment