Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, April 12, 2013

CHADEMA yatishia kujiengua mchakato wa katiba TZ


Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA na msemaji mkuu wa kambi ya upinzani katika Bunge la Tanzania
Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania (Chadema), kimesema huenda kikachukua uamuzi mzito wa kujiengua kwenye mchakato wa kutafuta  katiba mpya  nchini humo iwapo mambo muhimu  na ya kimsingi hayatapatiwa ufumbuzi wake hadi ifikapo tarehe 30 Aprili mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania imeeleza kuwa, Chadema kinataka kufutwa uteuzi au uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wanachi wa Kata bila ya  kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata. Wakati huohuo,
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) limesema kuwa, uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania haukuwa huru na uligubikwa na kasoro nyingi, na hivyo kupendekeza  urudiwe katika maeneo yaliyokuwa na utata.

No comments:

Post a Comment