skip to main |
skip to sidebar
Watu 20 wauawa katika machafuko C.A.R.
Watu wasiopungua 20 wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na
makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kuzuka machafuko katika mji mkuu
wa nchi hiyo Bangui. Duru za hospitali, polisi na mashuhuda wanasema
kuwa, watu hao wameuawa katika mapigano na machafuko tofauti yaliyotokea
katika mji wa Bangui. Taarifa zaidi zinasema kuwa, watu 12 wameuawa
katika Wilaya 7 za mji mkuu Bangui huku Shirika la Msalaba Mwekundu
likiongeza kuwa, watu wengine wanne wameuawa katika maeneo mengine ya
mji huo. Polisi imesema kuwa, mapigano hayo yalizuka wakati wanachama wa
muungano wa waasi wa Seleka walipokuwa wakisaka silaha baina ya raia.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Baraza la Mpito katika Jamhuri ya
Afrika ya Kati limemuidhinisha kiongozi wa kundi la SELEKA, Michel
Djotodia kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo. Baraza hilo lenye wanachama
105 limemuidhinisha baada ya kukosekana mpinzani. Mwezi uliopita,
Djotodia aliwaongoza waasi wa SELEKA kuipindua serikali ya Rais Francois
Bozize ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Benin.
Na Salum Bendera
No comments:
Post a Comment