Mafuriko yaliyoikumba Luanda mji mkuu wa Angola yameuwa watu
wasiopungua tisa na wengine wanne hawajulikani walipo. Watu hao
walipoteza maisha baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua kali
zilionyesha juzi huko Luanda mji mkuu wa Angola. Miongoni mwa wahanga wa
mafuriko hayo ni watoto. Shirika la habari la utangazaji la Angola
(Angop) limeripoti kuwa mafuriko hayo ya juzi yamebomoa mamia ya nyumba
za raia na kusababisha hasara kubwa ya mali. Limesema nyumba 500
zimebomoka katika maeneo ya Samba na Coreia pekee mjini Luanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment