Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, April 21, 2013

Wabahrain wapinga mashindano ya langa-langa


Waandamanaji Bahrain wakiwa na vibonzo vinavyoonyesha namna mashindano ya langa-langa yatakavyosaidia ukandamizajiVikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kufanyika mashindano ya magari ya langa-langa ya Formula One Grand Prix ambayo yanatazamiwa kuanza leo katika mji mkuu, Manama.
Watu wa Bahrain wanataka mashindano hayo yasimamishwe kwa sababu utawala wa ukoo wa Aal Khalifa unakandamiza maandamano ya amani ya wanaotaka mabadiliko nchini humo. Wabahrain wanasema utawala wa kifalme unataka kutumia mashindano hayo ya langa-langa kuonyesha kila kitu ni shwari katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Kwa miaka miwili sasa Bahrain imekumbwa na mgogoro mkubwa uliosababisha mashindano hayo ya magari yasifanyike mwaka 2011. Mwaka 2012 utawala wa Aal Khalifa ulifanya mashindano hayo kwa kustafidi na uungaji mkono wa vikosi vya usalama vya Saudia. Lakini mwaka huu wananchi na wapinzani wa Bahrain wamesisitiza kuendelea na malalamiko yao dhidi ya hatua kama hizo za kimaonyesho, licha ya ukandamizaji wa utawala wa kifalme wa Aali Khalifa.

No comments:

Post a Comment