Serikali ya Ghana imeondoa ruzuku ya
bidhaa za fueli yakiwemo mafuta ya petroli, mafuta ya dizeli na gesi
ili kusaidia kupunguza nakisi katika bajeti yake. Uamuzi huo umetangazwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Taifa ya Bidhaa za Petroli (NPA)
Alex Mould ambaye amesisitiza kuwa utekelezaji wa uamuzi huo umeanza
rasmi leo. Kutokana na kuchukuliwa hatua hiyo bei ya mafuta ya petroli
itapanda kwa asilimia 3 na bei ya mafuta ya dizeli kwa asilimia 2. Ghana
imekuwa moja ya nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani tangu
ilipoanza kuzalisha mafuta mwaka 2010, lakini serikali imekuwa
ikikabiliwa na changamoto ya kudhibiti nakisi ya bajeti ya matumizi yake
na uthabiti wa sarafu ya nchi hiyo ya cedi. Nakisi ya bajeti ilifikia
kiwango asilimia 12.1katika mwaka uliopita wa 2012 mara mbili zaidi ya
lengo lililowekwa la asilimia 6.7. Uamuzi wa kuondoa ruzuku katika
bidhaa za fueli ulikuwa utekelezwe tangu mwaka uliopita nchini Ghana
lakini ulicheleweshwa kwa sababu ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi
Disemba kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Atta Mills…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment