Askari polisi na wanajeshi wa Misri hawatashiriki kwenye uchaguzi
wowote hadi mwaka 2020. Bunge la Misri limesitisha hadi mwaka 2020
mpango wa kuwapa wanajeshi na askari polisi wa nchi hiyo haki ya kupiga
kura. Awali Naibu Waziri wa Ulinzi anayehusika na masuala ya sheria na
katiba wa Misri alitoa pendekezo kwa kamati ya bunge la nchi hiyo
kuandaa mpango wa kuwapatia wanajeshi na askari polisi haki ya kupiga
kura kwenye chaguzi mbalimbali zitakazofanyika nchini humo. Mahakama ya
Katiba ya Misri mwezi Mei mwaka huu ilitangaza kuwa, kwa mujibu wa
katiba mpya ya nchi hiyo, askari polisi na wanajeshi wana haki ya
kushiriki kwenye chaguzi nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment